Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 15:16

Zamaleck yaendeleza ushindi dhidi ya Espoir Fukash ya DRC

Anas Mahmoud wa Zamalek akiweka mpira nyavuni kwa dunki dhidi ya BC Espoir Fukash Aprili 16, 2022 .Picha na Armand Lenoir/NBAE kupitia Getty .
Anas Mahmoud wa Zamalek akiweka mpira nyavuni kwa dunki dhidi ya BC Espoir Fukash Aprili 16, 2022 .Picha na Armand Lenoir/NBAE kupitia Getty .

Zamalek ya Misri ilijikatia tikiti ya kutetea taji lao katika msimu wa ligi ya mpira wa vikapu Afrika wa 2022 kwa ushindi wao wa nne katika mkutano wa Nile baada ya kuwalaza ESPOIR FUKASH ya DRC 101-92 mjini Cairo Jumamosi.

Zamalek walianza kwa kasi kwa pointi tatu za iIke Diogu.

Mikh Mckinney aliongeza nyingine mbili baada ya kukimbia katikati na kuweka mpira nyavuni.

Espoir ilipambana vikali kusalia kwenye mchezo huku Nel akiruka na kuweka mpira nyavuni kabla ya muda kumalizika.

Lakini vijana wa Zamalek waliongeza uongozi wao kwa pointi tatu za Eslam Mohammed kabla ya Espoir kujibu na tatu zao kutoka kwa Kabuya.

Naye Ambanza wa Espoir alikamata pasi mbaya kutoka kwa Zamalek iliyopelekea Fula Nganga kupachika mpira nyavuni.

Mahmoud aliifungia Zamalek baada ya kupokea pasi ya juu na kuruka na mpira kupachika nyavuni uliotoka kwa Mckinney, na Wamisri wakaendeleza uongozi kwa pointi tatu kutoka kwa Eslam Mohamed nusu ya mchezo katika kota ya tatu.

Fula Nganga alijibu kwa point tatu kwa Espoir baada ya kupokea pasi ya Kabuya.

Mckinney aliweka tena mpira nyavuni na kuipa Zamalek pointi nyingine mbili.

Vijana wa DRC Espoir Fukash walipambana vikali kutaka kurejea mchezoni kwa pointi tatu za dakika za mwisho za Kabuya lakini muda ulizidi kuyoyoma kwa timu hiyo ya DRC ambayo ilipoteza mchezo wao wa kanda hiyo ya Nile.

XS
SM
MD
LG