Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 02:28

Zaidi ya Watu 45 wauwawa Mpeketoni Kenya


Wanajeshi wa Kenya washika zamu kwenye uwanja mdogo wa ndege wa Garrisa
Miili ya watu 48 ziliweza kupatikana alfajiri ya Jumatatu kufuatia mapigano ya saa kadhaa Jumapili usiku katika mji wa mapumziko wa Mpeketoni, kaskazini mashariki ya Kenya kufuatia shambulizi lililofanywa na wapiganaji wanaodhaniwa kuwa ni wa kundi la Kisomali la Al Shabab.

Kufuatana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya, miili ya watu 48 imeweza kupatikana idadi iliyothibitishwa pia na mkurugenzi wa mawasiliano wa wizara ya mambo ya ndani ya Kenya Mwenda Njoka.

Watu wenye silaha nzito nzito waklishambulia migahawa, hoteli, majengo ya serikali na vituo vya polisi na kupambana na vikosi vya usalama kwa saa kadhaa kabla ya kukimbia.

Maafisa wa usalama wa Kenya wanasema inakadiriwa kulikuwa na washambulizi karibu 50 ndani ya magari matatu walokuwa wanapeperusha bendera ya Al-Shabaab walipoinguia katika mji huo uliyoko karibu na Lamu na kukabiliwa na mapambano makali kutoka maafisa wa usalama waa Kenya.

Maafisa wanasema wapiganaji hao walipokimbia walitia moto kituo cha polisi na hoteli 3 katika mji huo, na hadi tunapoandika makala haya maafisa wa Msalaba Mwekundi wameripoti kwamba wafanyakazi wake wangali wanatafuta waathiriwa.

Inaripotiwa kwamba migahawa na baa zilikua zimejaa watu walokuwa wanatizama michuano ya Kombe la Dunia iliyokua inaendelea Brazil, wakati mashmabulizi yalipoanza Mpeketoni mji kwenye pwani ya Kenya kilomita 30 kusini magharibi wa kisiwa cha Lamu.
XS
SM
MD
LG