Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 18:21

Zaidi ya wapiganaji 400 wa zamani wapokonywa silaha Sudan.


Wanajeshi wa Syudan Kusini katika gwaride.
Wanajeshi wa Syudan Kusini katika gwaride.

Zaidi ya wapiganaji 400 wa zamani wapokonywa silaha Sudan na kurudishwa kwenye jamii..

Kikosi cha umoja wa mataifa huko Darfur Sudan (UNAMID) kimesema kimeanza kampeni ya kuwapokonya silaha na kuwarudisha kwenye jamii zaidi ya wapiganaji 400 wa zamani kutoka pande zote mbili kati ya waasi na serikali.

Umoja wa mataifa umesema umeanza kampeni jumatatu huko El Fasher kaskazini mwa Darfur na wapiganaji kutoka pande zote za majeshi ya Sudan na makundi kadhaa ya waasi.

Washiriki watafanyiwa uchunguzi wa usalama, afya zao na uchunguzi wa kisaikolojia . Mpango huo pia unahusisha warsha juu ya namna ya kuwarudisha upya kwenye jamii, kuwafundisha mbinu za kazi na fedha za posho ili kusaidia wapiganaji wa zamani kuweza kurudi kwenye jamii.

XS
SM
MD
LG