Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Agosti 24, 2026 Local time: 09:11

Zaidi ya wahamiaji 400 wamefariki katika miezi mitatu ya kwanza ya 2023 katika bahari ya Mediterania-IOM

Nembo ya IOM, shirika la Kimataifa linaloshughulikia wahamiaji
Nembo ya IOM, shirika la Kimataifa linaloshughulikia wahamiaji

Miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2023 ilikuwa ya maafa makubwa katika miaka sita kwa wahamiaji ambao wanavuka bahari ya Mediterania ndani ya boti za walanguzi, shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji limeripoti Jumatano.

Shirika hilo la kimataifa la uhamiaji lilirekodi vifo 441 vya wahamiaji kwenye njia hatari kati ya Afrika Kaskazini na mwambao wa kusini mwa Ulaya katika miezi ya Januari, Februari, na Machi.

Mwaka 2017, vifo 742 vilivyojulikana vilirekodiwa katika kipindi hicho, huku 446 vikirekodiwa katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2015.

“Mzozo wa kibinadamu unaoendelea katika eneo la kati la Mediterania hauwezi kuvumiliwa,” mkurugenzi mkuu wa IOM Antonio Vitorino, alisema kuhusu takwim zilizotolewa katika ripoti ya shirika hilo.

Wakati mwaka huu umeanza kwa hali ya kutatanisha, IOM ilihesabu idadi kubwa zaidi ya watu waliokufa au kutoweka katika bahari ya Mediterania katika robo nyingine sita tangu mwaka wa 2017, huku vifo vingi vilivyorekodiwa katika robo ya pili ya 2018, vikiwa 1,430.

XS
SM
MD
LG