Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 21, 2025 Local time: 00:45

Zaidi ya wafungwa 1,000 waachiliwa huru Sri Lanka wakati wa Siku Kuu ya Krismasi


Baadhi ya dawa za kulevya zilizonaswa kwenye msako wa Sri Lanka. Picha ya maktaba.
Baadhi ya dawa za kulevya zilizonaswa kwenye msako wa Sri Lanka. Picha ya maktaba.

Rais wa Sri Lanka, Ranil Wickremesinghe ametoa msamaha kwa zaidi ya wafungwa 1,000 waliofungwa jela kote nchini, kama sehemu ya maadhimisho ya Krismasi, afisa mmoja wa magereza amesema Jumatatu.

Miongoni wa wafungwa 1,004 walioachiliwa ni wale walioshindwa kulipa faini, kulingana na kamishna wa magereza Gamini Dissanayake. Idadi kubwa ya watu wa Sri Lanka ni wa Budha, na idadi sawa na hiyo ya wafungwa iliachiliwa Mei, wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya Vesak, inayosherehekea siku ya kuzaliwa kwa Budha, kutawazwa kwake, pamoja na kifo.

Msamaha wa Jumatatu umekuja baada ya polisi kukamata zaidi ya watu 15,000 kwenye msako wa wiki nzima wakisaidiwa na jeshi dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya, wakati ukisitishwa kwenye mkesha wa Krismasi.

Taarifa ya polisi imesema kwamba washukiwa 13,666 walikamatwa wakati karibu 1,100 wakiwa ni waraibu wa dawa za kulevya, ambao walitiwa mbaroni na kupelekwa kwenye vya ukarabati kwenye kituo kinachoendeshwa na jeshi.

Kufikia Ijumaa, taifa hilo lilikuwa na karibu wafungwa 30,000, kwenye magereza yenye uwezo wa kuwashikilia watu 11,000 pekee, kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa.

Forum

XS
SM
MD
LG