Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 06:09

Zaidi ya raia 150 wa Korea Kusini wamefariki kwa mkanyagano


Timu ya uokozi na wafanyakazi wa zimamoto wakiwa eneo la tukio lililosababisha zaidi ya watu 150 kufariki mjini Seoul
Timu ya uokozi na wafanyakazi wa zimamoto wakiwa eneo la tukio lililosababisha zaidi ya watu 150 kufariki mjini Seoul

Raia wa Korea Kusini wanatafuta majibu wakati nchi hiyo ikiomboleza baada ya zaidi ya watu 150 kufariki katika mkanyagano wakati wa tamasha la Halloween katika wilaya maarufu kwa hafla

Raia wa Korea Kusini wanatafuta majibu wakati nchi hiyo ikiomboleza baada ya zaidi ya watu 150 kufariki katika mkanyagano wakati wa tamasha la Halloween katika wilaya maarufu kwa hafla.

Maafisa walisema watu 82 pia walijeruhiwa katika tukio hilo la Jumamosi usiku katika eneo la Itaewon mjini Seoul, ambalo lilikuwa limejaa umati wa watu kabla ya sikukuu ya Jumatatu.

Ni tukio baya sana la mkanyagano wa watu wengi katika historia ya Korea Kusini. Maafisa wanasema wengi wa waathirika walikuwa vijana katika umri wao wa ujana hadi miaka ishirini hivi.

Haikufahamika mara moja kilichochochea mkanyagano huo, ambao ulianza kwenye njia nyembamba iliyojaa vilabu.

XS
SM
MD
LG