Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:22

Zaidi ya Majaji 40 wapewa mafunzo Tanzania


Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Tanzania Jaji Damian Lubuva
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Tanzania Jaji Damian Lubuva

Waratibu wa mafunzo hayo ya majaji na wasajili wa mahakama kuu nchini ni mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania THRDC walioshitushwa na kasi ndogo ya kushughulikia mashauri katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2010

Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania Jumanne zaidi ya majaji arobaini wa mahakama kuu na wasajili wa mahakama wamekutana jijini Dar es Salaam katika mafunzo yanayolenga kuwajengea uwezo wa kuyafanyia kazi kwa haraka na kwa wakati mashauri yatakayotokana na kesi zinazohusiana na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 25 mwaka huu.

Mafunzo ya majaji Tanzania
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:23 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Waratibu wa mafunzo hayo ya majaji na wasajili wa mahakama kuu nchini ni mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania THRDC walioshitushwa na kasi ndogo ya kushughulikia mashauri katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2010.

Mafunzo ya majaji Tanzania
Mafunzo ya majaji Tanzania

ambapo jumla ya mashauri 44 yanayohusiana na uchaguzi mkuu yalifunguliwa lakini hata hivyo ni mashauri 17 tu ndiyo yaliyofanyiwa kazi na kufikia mwisho

Mohamed Chande Othman - Jaji Mkuu wa Tanzania, amesema uchaguzi wa mwaka huu una changamoto zaidi na mafunzo kwa majaji na wasajili yamekuja wakati muafaka zaidi, kauli iliyoungwa mkono pia na mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi jaji mstaafu Damian Lubuva.

XS
SM
MD
LG