Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:12

YouTube yaondoa mamilioni ya video zenye taarifa za kupotosha


 Nembo ya kampuni ya YouTube
Nembo ya kampuni ya YouTube

Mtandao wa Youtube Jumatano umesema umeondoa kwenye mtandao wake zaidi ya video millioni moja za habari hatari za kupotosha kuhusu virusi vya corona, tangu kutokea kwa hilo mwaka iliyopita.

Taarifa ya mtandao huo unaomilikiwa na kampuni ya Google, inajiri wakati mitandao ya kijamii ikishutumiwa vikali na viongozi wa kisiasa kutokana na kushindwa kudhibiti usambazaji wa habari potofu kuhusu virusi vya corona pamoja na mada nyingine.

Youtube imesema katika taarifa kwenye blogi yake kwamba inategemea maelezo ya wataalamu wa afya, ikiwemo kituo cha kudhibiti magonjwa hapa Marekani (CDC) na shirika la afya duniani (WHO), lakini imekuta wakati mwingine kwamba, si rahisi kutambua habari potofu, wakati ukweli mpya unaibuka.

“Sera zetu zinaangazia kuondoa video za aina yoyote ambazo zinaweza kusababisha madhara mabaya kwa ulimwengu,” afisa mkuu anaehusika na bidhaa, Neal Mohan ameandika.

XS
SM
MD
LG