Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:51

Yemen: upinzani wataka baraza la mpito kuchagua serikali mpya


Waandamanaji wa kuipinga serikali wakidai rais wa Yemen kujiuzulu
Waandamanaji wa kuipinga serikali wakidai rais wa Yemen kujiuzulu

Vyanzo vya kidiplomasia zilieleza Jumanne kwamba asilimia 40 ya mwili wa kiongozi huyo inamajeraha kutokana na moto ikiwa ni pamoja na uso, shingo na kifua.

Wafuasi wa upinzani wanaoipinga serikali ya Yemen wanamhimiza kaimu kiongozi wa nchi hiyo kuunda baraza la mpito ambalo litaunda serikali mpay wakati rais Ali Abdulah Saleh anatibiwa majeraha nchini Saudi Arabia.

Maandamanao yaliendelea Jumatano nje ya makazi ya makamu wa rais Abd al-Rab Mansur Hadi katika mji mkuu wa Sana’a. Hata hivyo wanajeshi walifanikiwa kwenda na kuondoa hema zilizokuwa zimesimikwa nje ya nyumba na baadhi ya waandamanaji.

Wakati huo huo maafisa wanasema Bw. Saleh anaendelea vizuri na matibabu kutokana na majeraha aliyopaya kufuatia shambulizi la roketi katika makazi ya rais wiki iliyopita.

Maafisa wa Yemen awali walisema bwana Saleh alijeruhiwa na mabaki ya roketi. Hata hivyo maafisa wa Marekani na Yemen baadae wamesema majeraha yake ni makubwa kuliko ilivyoelezwa.

Vyanzo vya kidiplomasia zilieleza Jumanne kwamba asilimia 40 ya mwili wa kiongozi huyo inamajeraha kutokana na moto ikiwa ni pamoja na uso, shingo na kifua. Inaaminika alipata jeraha kubwa kichwani.

Maandamano ya kuipinga serikali yanaendelea licha ya kwamba rais hayuko nchini. Kulikuwepo na mapigano zaidi Jumanne katika mji wa pili kwa ukubwa wa Taiz. Na wanajeshi wa serikali walipambana na wanamgambo katika mji wa kusini wa Zanjibar.

XS
SM
MD
LG