Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 01:32

UNHCR yapeleka msaada Yemen


Raia wa Yemen wakibeba msaada walopokea huko mjini Taiz, Yemen
Raia wa Yemen wakibeba msaada walopokea huko mjini Taiz, Yemen

Mji wa Taiz umekumbana na mapigano makali katika kipindi cha miezi 10 ilopita.

Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbi – UNHCR, limepeleka vifaa vya dharura vinavyohitajika sana na maelfu ya watu katika mji wa Taiz nchini huko Yemen.

Baada ya zaidi ya wiki tatu za majadiliano, idara ya wakimbizi ya umoja mataifa iliweza kuingia mji wa Taiz siku ya Jumapili. Idara hiyo imepeleka mablanketi, magodoro na msaada mwingine wa dharura kwa familia takriban elfu moja ziloathiriwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Yemen.

Mji wa Taiz umekumbana na mapigano makali katika kipindi cha miezi 10 ilopita.

Waasi wa Houthi walizuia msaada mwingi wa kibinadamu kufikia wakazi takriban laki 2, kwa takriban miezi 6.

Msemaji wa UNHCR Andreas Needham anasema mwakilishi wa idara hiyo Johannes Van Der Klaauw, alisimamia usambazaji wa msaada na kushuhudia mahitaji muhimu ya watu ambao wamenyimwa msaada wa kuokowa maisha yao.

Anaiambia VOA kuwa, Van Der Klaauw anataraji msaada huo, hautokuwa shughuli ya mara moja tu.

Amesema anatumaini kuwa hilo litakuwa ndio chanzo cha uwezekano wa kufikisha kila aina ya msaada na itajumlisha washirika wetu wa UNHCR, kama vile WHO, na ICRC. Pia alirudia wito wa kupatikana njia wazi kwa wote wanaopeleka msaada wa kibinadam.

Wiki ilopita, shirika la afya duniani WHO, lilifikisha Zaidi ya tani 20 ya vifaa vya afya huko Taiz. Msemaji wa WHO Fadela Chaib, anasema hali mjini humo inatisha.

Hospitali nyingi zimelazimishwa kufunga wodi zao za wagonjwa mahututi kutokana na ukosefu wa mafuta, dawa, na wafanyakazi wa afya na wagonjwa wenye magonjwa sugu , kama vile kisukari, magonjwa ya figo na saratani, wanahangaika kupata dawa.

Chaib anasema WHO inataraji kusambaza takriban tani 40 za dawa na vifaa vya afya kote nchini katika wiki zijazo.

XS
SM
MD
LG