Kissinger mwenye umri wa miaka 100 anaheshimika China kutokana na jukumu lake katika kuanzisha mahusiano kati ya chama cha Kikomunisti cha China na Washington, chini ya utawala wa Rais wa zamani wa Marekani Richard Nixon wakati wa kipindi cha vita baridi mwanzoni mwa miaka ya 70.
Xi ambaye ni kiongozi wa taifa, katibu mkuu wa chama na pia kamanda wa jeshi kubwa zaidi ulimwenguni amekutana na Kissinger kwenye kikao kisicho rasmi katika nyumba ya wageni ya serikali ya Diayutai mjini Beijing, akiandamana na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa taifa hilo Wang Yi.
Ziara ya Kissinger imefayika wakati mmoja na mjumbe wa ngazi ya juu wa hali hewa wa Marekani John Kerry, akiwa afisa wa 3 wa ngazi ya juu kwenye utawala wa Biden kuitembelea China katika wiki za karibuni. Wengine ni waziri wa mambo ya nje wa Marekani na waziri wa fedha Janet Yellen.
Forum