Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 11:55

Viongozi tayari kwa mikutano ya G-8 na G-20 Canada


Viongozi na maafisa wakiwasili Canada tayari kwa mikutano ya G-8 na G-20.
Viongozi na maafisa wakiwasili Canada tayari kwa mikutano ya G-8 na G-20.

Viongozi duniani wawasili Canada tayari kwa mikutano ya G-8 na G-20 mjini Toronto..

Viongozi wa dunia wanakusanyika Toronto, Canada, tayari kwa mikutano miwili ya nchi zenye viwanda vikubwa na mataifa yanayoongoza katika nchi zinazoendelea.

Marais na mawaziri wakuu walianza kuwasili Toronto Alhamisi kwa ajili ya mikutano ya G-8 na G-20, ikiwa ni pamoja na Rais Dmitri Medvedev wa Russia, Waziri Mkuu wa Japan Naoto Kan na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron.

Katika makala iliyochapishwa kwenye gazeti la Globe and Mail, kiongozi wa Uingereza alisema mikutano hiyo inahitaji kuwa zaidi ya "mazungumzo" na badala yake ihakikishe maendeleo yanapatikana katika maswala muhimu ya uchumi wa dunia.

Maafisa wanasema viongozi hao watajadili maswala ya usalama lakini sehemu kubwa ya mazungumzo itatilia mkazo njia za kuhakikisha ukuaji uchumi na kupambana na nakisi za bajeti. Rais Barack Obama wa Marekani anatazamiwa kuwasili Toronto Ijumaa.

XS
SM
MD
LG