Umoja wa wafanya kazi wa petroli na gesi wa Nigeria, Pengassan, unasema majeshi ambayo yametumwa kwenye eneo la Niger Delta kulinda miundo mbinu na vinu vya petroli ndiyo kiini dhidi ya jitihada za kutokomeza wizi wa petroli.
Rais wa Umoja wa Pengassan, Festus Osifo anasema serekali ni lazima ichukue hatua madhubuti kwa wote wanaohusika kwenye wizi huo, unaorudisha nyuma maendeleo ya taifa. Ameongeza kusema kwamba wanajeshi na maafisa wa usalama wanaotumwa kulinda vituo vya petroli huko Niger Delta, wanashirikiana na wenyeji pamoja na wahalifu katika kuendeleza uovu huo.
Utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa Nigeria inapoteza mapipa 700,000 ya mafuta kila siku na wala haijaweza kutoa mgao wa OPEC wa mapipa milioni 1.8 kila siku kama inavyohitajika.