Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:09

Wizara ya utalii Kenya yajadili mkakati wa kuboresha utalii Mombasa


Bidhaa zilizotengenezwa kwa mikono kama sehemu ya utalii nchini Kenya.
Bidhaa zilizotengenezwa kwa mikono kama sehemu ya utalii nchini Kenya.

Mji wa Mombasa nchini Kenya unatambulika ulimwenguni kote kutokana na mandhari yake yanayowavutia watalii kutoka mataifa mbalimbali.

Wizara ya utalii ya Kenya imekuwa ikifanya kila juhudi kuhifadhi sifa za mji huo kiutalii ili kukuza sekta ya utalii inayotajwa kuchangia pato kubwa kwa uchumi wa taifa la kenya.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:38 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Waziri wa utalii wa Kenya bwana Najib Balala alikutana na wadau wa sekta ya utalii nchini humo ili kujadili mikakati ya kuboresha utalii katika eneo la Mombasa kwa ushirikiano na serikali za ugatuzi. “Tutafanya kazi kwa ushirikiano na serikali za kaunti, baadae tutakutana na magavana wote ili kuzindua bidhaa mbali mbali za kitalii zinazopatikana katika kaunti zao na hiyo ni hatua nzuri sana ambayo tumechukua hii leo, kwa hiyo tunatengeneza ushirikiano, ushirikiano ambao serikali kuu itatekeleza majukumu yake, serikali za kaunti zitatekeleza majukumu yake na pia tuko na mashirika ya kibinafsi kila mtu afanye majukumu yake”.

Katika siku za hivi karibuni sekta hiyo ilikumbwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kudorora kwa usalama miongoni mwa changamoto zingine.

XS
SM
MD
LG