Kwenye video iliyovuja, Popov anailaumu wizara ya Ulinzi ya Russia kwa kushambulia jeshi kutoka upande wa nyuma wakati ambapo linahitaji uungaji mkono wa kila mmoja.
Kwenye taarifa ya kila siku kutoka kwa wizara ya Ulinzi ya Uingereza, malalamiko kutoka kwa maafisa wa jeshi la Russia yanaendana na yale yaliotolewa na mmiliki wa kundi la Wagner Yevgeny Prigozhin kabla ya kuongoza uasi mwezi uliopita.
Wakati huo huo mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya Ijumaa wamekubaliana kuhusu kuongezwa kwa misaada ya kifedha kwa Ukraine. EU imependekeza kuongezwa dola bilioni 74.1 kwa ajili ya Ukraine hadi 2027.
Forum