Idara hiyo ya uchunguzi wa mizozo “itafuatilia, kuchambua, na kutoa ushahidi wa kutosha unaopatikana kuhusu uhalifu wa kivita na ukatili unaotekelezwa na Russia nchini Ukraine,” wizara ya mambo ya nje imesema.
Idara hiyo itakusanya taarifa zinazopatikana hadharani na kibiashara, ikiwemo yale yanayoonekana kwenye mitandao ya kijamii na picha za kibiashara za satelaiti, kwa ajili ya matumizi katika utaratibu wa kisheria wa makosa ya jinai wa sasa na wa baadaye.
Karibu miezi mitatu tangu Russia iivamie Ukraine, Kyiv inasema imebaini maelfu ya visa vinavyoshukiwa kuwa uhalifu wa kivita.
Kubwa zaidi ni madai ya mauaji ya kiholela ya raia wengi katika mji wa Bucha, nje kidogo ya Kyiv.
Idara hiyo itaunda jukwa la mtandaoni ili kusaidia kukanusha juhudi za Russia kutoa taarifa potofu na kuangazia unyanyasaji,” wizara ya mambo ya nje imesema.