Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 20:48

WHO yatangaza kumalizika kwa maambukizo ya Ebola Guinea


Wafanyakazi wa huduma za afya wakishughulikia wagonjwa wa Ebola
Wafanyakazi wa huduma za afya wakishughulikia wagonjwa wa Ebola

Shirika la faya duniani WHO jana lilitangaza kumalizika kwa maambukizo ya Ebola nchini Guinea, baada ya taifa hilo la Afrika Magharibi kuvuka siku 42 bila kuwa na kesi zilizothibitishwa za ugonjwa huo hatari.

Guinea kwa mara ya kwanza ilitangazwa kuwa huru kutokana na Ebola hapo December. Tangu wakati huo imekuwa na kesi 2. Taifa hilo la Afrika Magharibi sasa limepitisha vipindi viwili vya siku 21 bila kuwa na kesi ya Ebola. Kwa hiyo shirika la afya duniani WHO linaitangaza Guinea kuwa huru kutokana na Ebola kwa mara ya 2.

Msemaji wa WHO Christian Lindmeir ameiambia sauti ya America kuwa kile Guinea inachoshuhudia sio jambo lisilo la kawaida. Anaelezea wote Liberia na Sierra Leone pia zimekuwa na mlipuko ya maradhi tangu kutangazwa kuwa hazina ebola.

Bw Lindmeir anasema,tunabidi tutarajie kuibuka kwa kesi za hapa na pale. Hili limesemwa hapo awali na tumeona likitokea , lakini kwa vile nchi sasa zimejiandaa , tunaimani kuwa kesi hizi zitaweza kushughulikiwa kwa haraka na kwa ufanisi. Lakini tukiangazia mbele Zaidi, iwapo siku hizi zote 90 zikipita basi maambukizo ya Ebola yatangazwa kuwa yamekwisha.

Katika mlipuko wa hivi karibuni, kesi 7 zilithibitishwa na kesi nyengine 3 za Ebola ziloripotiwa baina ya March 17 na Aprili 6. Guinea sasa inaingia kipindi cha siku 90 za ufuatialiaji wa karibu sana ili kuhakikisha kesi zozote mpya zinatambuliwa haraka kabla kusambaa kwa watu wengine.

Zaidi ya watu elfu 11 wamefariki kutokana na Ebola katika mataifa 3 yalioathiriwa huko Afrika Magharibi, wakati WHO ilipotangaza maambukizo ya virusi vya Ebola kuwa imekwisha mwishoni mwa mwaka jana. Zaidi ya vifo elfu 2 mia 5 vilitokea huko Guinea.

XS
SM
MD
LG