Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 20:48

WHO yazidi kuelezea khofu ya kusambaa Ebola Afrika


Mkurugenzi wa WHO Margaret Chan akiwa washington DC akizungumzia juu ya khofu ya kusambaa Ebola, Sept. 3, 2014.
Mkurugenzi wa WHO Margaret Chan akiwa washington DC akizungumzia juu ya khofu ya kusambaa Ebola, Sept. 3, 2014.

Shirika la afya duniani katika Umoja wa Mataifa linatoa wito kwa ushirikiano wa ulimwengu kujibu mapambano ya ongezeko la mlipuko wa Ebola unaoathiri maeneo kadhaa katika mataifa ya Afrika magharibi.

Margaret Chan, mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani- WHO, alisema jumatano kwamba mlipuko hadi sasa umeuwa zaidi ya watu 1,900 na uliambukiza watu wasiopungua 3,500 katika eneo hilo. WHO inakadiria kwamba itagharimu hadi dola milioni 600 kukabiliana na mlipuko huu.

Wakati huo huo Tom Kenyon, mkurugenzi wa kitengo cha afya kwenye kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa nchini Marekani-CDC anasema virusi hivyo vinasambaa sana na kwamba muda wa kupambana na ugonjwa huo unakwisha.

Maafisa wa afya wa Marekani wanasema jambo kuu la kudhibiti mlipuko litakuwa kuongeza idadi ya vituo vya matibabu ya Ebola, kutoa vifaa vya kujikinga kwa wafanyakazi wa afya na kuwafuatilia wale waliokuwa na mawasiliano na watu walioambukizwa.

Wataalamu wa afya wanaonya kwamba Ebola itaweza kusambaa zaidi ya mataifa hayo matano yalioathiriwa huko Afrika magharibi: Guinea, Liberia, Nigeria, Senegal na Sierra Leone.

XS
SM
MD
LG