Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 15:38

WHO yaonya nchi jirani baada ya kufika  kwa Ebola Kampala


Madaktari wakiuwa vijidudu baada ya kumtembelea mgonjwa ambaye alikuwa akiwasiliana na mwathiriwa wa Ebola, Alhamisi, Oktoba 20, 2022, huko Entebbe, Uganda.(AP)
Madaktari wakiuwa vijidudu baada ya kumtembelea mgonjwa ambaye alikuwa akiwasiliana na mwathiriwa wa Ebola, Alhamisi, Oktoba 20, 2022, huko Entebbe, Uganda.(AP)

Shirika la Afya Duniani lilionya Jumatano kwamba kufika  kwa Ebola katika mji mkuu wa Uganda kulionyesha hatari kubwa ya kuenea zaidi kwa virusi hivyo, likitoa wito kwa nchi jirani kuongeza utayari wao.

Tangu wizara ya afya ya Uganda itangaze mlipuko huo kwa mara ya kwanza Septemba 20, nchi hiyo imesajili zaidi ya visa 150 vilivyothibitishwa na vinavyowezekana, vikiwemo vifo 64, WHO ilisema.

Na tangu ugonjwa huo hatari kuenea Kampala wiki jana, kesi 17 zimethibitishwa huko, mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus aliwaambia waandishi wa habari.

Ingawa kesi hizi zinahusishwa na maeneo yanayojulikana, ukweli kwamba kuna kesi katika jiji lenye watu wengi unazidisha hatari halisi ya maambukizi zaidi, "alisema, akizungumza kutoka makao makuu ya WHO huko Geneva.

XS
SM
MD
LG