Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 16:23

WHO yaidhinisha chanjo mpya inayotumika kwa kiasi kikubwa  ya kipindu pindu


Familia moja ikiingia katika hema lililotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa kipindupindu katika kliniki moja mjini Harare, Zimbabwe, Novemba 18, 2023.
Familia moja ikiingia katika hema lililotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa kipindupindu katika kliniki moja mjini Harare, Zimbabwe, Novemba 18, 2023.

Shirika la Afya Ulimwenguni limeidhinisha toleo la chanjo mpya inayotumika kwa kiasi kikubwa  ya kipindu pindu

Shirika la Afya Ulimwenguni limeidhinisha toleo la chanjo inayotumika kwa kiasi kikubwa ya kipindu pindu ambayo inaweza kusaidia kukabiliana na ongezeko la kesi ambazo zimepunguza hifadhi ya chanjo ya kimataifa na kuziacha nchi maskini zikihangaika kudhibiti magonjwa ya milipuko.

WHO iliidhinisha chanjo hiyo, iliyotengenezwa na EuBiologics, ambayo pia inafanya utengenezaji huo kutumika sasa. Toleo jipya, linaloitwa Euvichol-S, ni fomula iliyorahisishwa ambayo inatumia virutubisho vichache, ni ya bei nafuu, na inaweza kufanywa kwa haraka zaidi kuliko toleo la zamani.

Chanjo hiyo ilionyeshwa kusaidia kuzuia ugonjwa huo wa kuhara katika hatua ya mwisho ya utafiti uliofanywa nchini Nepal.

Uidhinishaji wa WHO unamaanisha kwamba mashirika ya wafadhili kama muungano wa chanjo Gavi na UNICEF sasa wanaweza kununua chanjo hiyo kwa nchi masikini zaidi. Leila Pakkala, mkurugenzi wa kitengo cha ugavi cha UNICEF, alisema katika taarifa kwamba shirika hilo litaweza kuongeza usambazaji kwa zaidi ya asilimia 25.

Dk. Derrick Sim wa Gavi aliita idhini ya WHO njia ya kuokoa jamii zilizo hatarini ulimwenguni kote.

Forum

XS
SM
MD
LG