Viwango vya uvutaji sigara vinapungua, na maisha yanaokolewa wakati nchi nyingi zinatekeleza sera na hatua za kudhibiti kukabiliana na janga la tumbaku duniani, kulingana na ripoti ya Shirika la Afya Duniani iliyotolewa Jumatatu ambayo inapima maendeleo ya nchi katika udhibiti wa tumbaku.
Takwimu mpya zinaonyesha kupitishwa kwa mfuko wa WHO wa hatua sita za kudhibiti tumbaku miaka 15 iliyopita kumewalinda mamilioni ya watu kutokana na athari mbaya za matumizi ya tumbaku.
Hatua hizo ambazo zilizinduliwa mwaka 2008 zinatoa wito kwa serikali kufuatilia sera za matumizi ya tumbaku na kuzuia, kuwalinda watu dhidi ya moshi wa tumbaku, kutoa msaada wa kuacha matumizi ya tumbaku, kuwaonya watu kuhusu hatari za tumbaku, kuweka marufuku ya matangazo ya tumbaku, uhamasishaji na udhamini, na pia kuongeza kodi kwenye tumbaku.
Bila kiwango hiki kupungua kungekuwa na makadirio ya wavutaji tumbaku zaidi ya milioni 300 duniani hii leo, alisema Ruediger Krech, mkurugenzi wa matangazo katika shirika la afya duniani (WHO).
Forum