Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 15:25

WHO yaonya dhidi ya athari za ukeketaji kwa wanawake


Daktari wa kienyeji akishikilia wembe anaotumia kufanyia ukeketaji.

Kila mwaka shirika la afya duniani WHO, linaripoti kuwa takriban wasichana millioni 3 wengi wakiwa chini ya umri wa miaka 15 wanakabiliwa na ukeketaji.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:34 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Shirika la afya duniani WHO limetowa mwongozo wake wa kwanza kusaidia wafanyakazi wa afya kutowa huduma bora za kiafya na kisaikologia kwa zaidi ya wasichana na wanawake millioni 2 duniani kote waliokeketwa.

Kila mwaka shirika la afya duniani linaripoti kuwa takriban wasichana millioni 3 wengi wakiwa chini ya umri wa miaka 15 wanakabiliwa na ukeketaji. Idadi hio inaongezea ile ya wasichana na wanawake ambao tayari wanaishi na athari mbaya za kitendo hicho kiovu.

Ukeketaji wa wanawake unahusisha kukatwa sehemu au kuondolowe kabisa sehemu ya nje ya uke au kujeruhiwa kwa sehemu za uke kwa sababu zisizo za kiafya. Kitendo hichi kinafanyika sana katika nchi 30 za kiafrika na nchi kadhaa za Asia na Mashariki ya kati. Baada ya kuongezeka kwa uhamiaji duniani, kesi zaidi za ukeketaji zinafanyika huko Ulaya na Amerika ya kaskazini.

Mratibu wa idara ya afya ya uzazi na utafiti katika WHO Lale Say, anasema ukeketaji unaweza kusababisha matatizo kama vile maumivu, kutokwa kwa damu nyingi au hata kifo.

Bi Say anasema, kunahatari kubwa wakati wa uja uzito na kuzaa kwa mwanamke anayezaa, lakini pia ni hatari kwa mtoto wake. Inaweza kusababisha matatizo wakati wa kujifungua na hata kufariki kwa mtoto wakati wa kujifungua. Matatizo mengine ya kiafya pamoja na athari za kisaikologia.

WHO inasema kuwa wafanyakazi wa afya mara nyingi huwa hawana uwelewa wa athari mbaya za ukeketaji na hawajuwi jinsi ya kutibu. Idara hiyo ya afya inapendekeza kulenga juu ya kuzuia na kutibu matatizo ya uzazi na kuwasaidia wanawake wenye shida za kisakologia. Mwongozo pia unaonya dhidi ya matibabu ya ukeketaji.

Afisa wa afya wa WHO Doris Chou, anasema madaktari lazima wakatae maombi kutoka kwa wanafamilia kufanya ukeketaji, wakiamini kuwa si kitendo salama.

Bi Chou anasema, kimatibabu haikubaliki kwa sababu inakiuka maadili ya kiafya, kwa vile ni kitendo kiovu. Kimatibabu inaendeleza daima ukeketaji na athari zake zianzoshinda manufaa yanayodhaniwa. Kama watoaji huduma za afya, tunahitaji kujikumbusha kuwa tulichukuwa kiapo na nacho ni kutodhuru mtu.

WHO inasema mwongozo unaweza kusaidia juhudi zainazoendelea ulimwenguni za kutokomeza ukeketaji kwa kutowa maelezo bora kwa jumuiya ya kiafya kuhusu hatari nyingi zinazohusishwa na ukeketaji.

XS
SM
MD
LG