Ni mabadiliko makubwa sana katika sera huku White House ikikiri kuhusu ongezeko la wasi wasi kuhusu kusambaa kwa maambukizi zaidi ya virusi vya delta. Hatua ya kuwataka wapatiwe chanjo wafanyakazi wa serikali kuu ni njia moja ambayo inafikiriwa na utawala wa Biden.
White House inatarajiwa kutangaza maamuzi ya mwisho baada ya kukamilisha tathmini ya sera siku ya Alhamisi wiki hii.
Kwa mujibu wa tathmini kutoka ofisi ya Utawala na Bajeti ya serikali kuu, mwaka 2020 kulikuwa na zaidi ya wafanyakazi milioni 4.2 wa serikali kuu kote nchini, wakiwemo wale ambao wako katika jeshi.