Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 03:44

WFP kupeleka chakula Somalia


Wafanyakazi wa kutoa msaada wakijiandaa kusambaza mgao wa chakula kwenye kambi moja ya IDP mjini Mogadishu, Julai 25,2011
Wafanyakazi wa kutoa msaada wakijiandaa kusambaza mgao wa chakula kwenye kambi moja ya IDP mjini Mogadishu, Julai 25,2011

Shirika la chakula Duniani la Umoja wa Mataifa linaanza harakati za dharura kupeleka chakula katika maeneo yaliyokumbwa na ukame katika Pembe ya Afrika, Jumanne.

Shirika hilo lilisema Jumatatu kwamba ndege zitabeba chakula kuelekea mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, eneo la mashariki ya Ethiopia na Kaskazini ya Kenya, karibu na mpaka wake na Somalia.

Mkurugenzi mkuu wa WFP, Josette Sheeran alisema hii itakuwa mara ya kwanza kwa ndege kusafirisha chakula tangu Umoja wa Mataifa ulipotangaza baa la njaa katika maeneo mawili ya Somalia wiki iliyopita.

Umoja wa Mataifa unasema hatua za haraka zinahitajika kuokoa maisha ya mamilioni ya watu wanaoishi katika eneo la pembe ya Afrika na kutaabika na baa la njaa. Idara ya maendeleo ya kimataifa ya Marekani-USAID inasema zaidi ya watu milioni 11 hivi sasa wanahitaji msaada wa dharura ili waweze kuishi.
Idara ya
kilimo na chakula ya Umoja wa Mataifa ilifanya mkutano wa dharura juu ya ukame siku ya Jumatatu huko Rome.Yaripotiwa pia kuwa mkutano wa wafadhili utafanyika Jumatano katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Umoja wa Mataifa pia umesema unaomba msaada wa dola bilioni 1.6 ili kuwasaidia mamilioni ya watu wenye utapiamlo, wengi wao wakiwa watoto.

Somalia ilielezewa kama kiini cha baa la njaa, Sheeran alisema kiasi cha theluthi moja ya watu wanakabiliwa na baa la njaa nchini humo. Nalo shirika la USAID linaripoti kwamba zaidi ya wasomali 600,000 wamekimbia kuelekea nchi za jirani.

XS
SM
MD
LG