Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:06

Waziri wa Ulinzi wa Israel aelekea Morocco kwa ziara ya kuimarisha ushirikiano wao

Waziri wa ulinzi wa Israel Benny Gantz katika mkutano wa baraza la mawaziri.
Waziri wa ulinzi wa Israel Benny Gantz katika mkutano wa baraza la mawaziri.

Waziri wa Ulinzi wa Israel Benny Gantz anaelekea Morocco Jumanne kwa ziara ambayo itarasimisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, maafisa wanasema, wakati ambapo Rabat iko katika mzozo kuhusu Sahara Magharibi.

Ziara hiyo ya siku mbili inajiri chini ya mwaka mmoja baada ya Morocco kurekebisha uhusiano na Israel katika makubaliano yaliyosimamiwa na utawala wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.

Kutokana na makubaliano hayo Washington ilitambua mamlaka ya ufalme wa Afrika Kaskazini juu ya eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi.

Gantz, waziri wa kwanza wa ulinzi wa Israel kufanya ziara rasmi nchini Morocco, atatia saini mkataba wa maelewano ambao utaelezea ushirikiano wa kiulinzi kati ya nchi hizo mbili, ofisi yake ilisema.

Chanzo kinachofahamu ziara hiyo kiliiambia AFP kuwa safari hiyo inalenga kuweka msingi wa ushirikiano wote wa usalama wa siku zijazo kati ya Israel na Morocco, na chanzo hicho kiliongeza kuwa hadi sasa kumekuwa na kiwango fulani cha ushirikiano, hii inairasimisha kweli.

Morocco inadhibiti sehemu kubwa ya Sahara Magharibi na inachukulia koloni hilo la zamani la Uhispania kama eneo lake huru.

XS
SM
MD
LG