Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 07, 2025 Local time: 12:04

Waziri wa Ulinzi wa Israel adai kuwa Iran imejenga uwanja wa ndege ndani ya Lebanon ili kushambulia taifa lake


Gari la walinda amani wa UN likiwa kwenye mpaka wa Israel na Lebanon, karibu na kijiji cha Lebanon cha Marwaheen. Julai 12,2023.
Gari la walinda amani wa UN likiwa kwenye mpaka wa Israel na Lebanon, karibu na kijiji cha Lebanon cha Marwaheen. Julai 12,2023.

Waziri wa ulinzi wa Israel Yaov Gallant Jumatatu amelaumu Iran kwa kujenga uwanja wa ndege kusini mwa Lebanon, ili kuwezesha mashambulizi ya anga dhidi ya Israel.

Israel imekuwa na wasi wasi kutokana na Iran ambayo ni hasimu wake mkubwa kuendeleza program ya nyuklia, utengenezaji wa silaha pamoja na uungaji mkoni wa makundi yenye silaha ya kieneo. Moja wapo ya makundi hayo ni lile la Hezbollah kutoka Lebanon, na ambalo lilipigana vita na Israel 2006. Mwaka huu kumekuwa na matukio mengi ya kichokozi yaliyofanyika kwenye mpaka wa Israel, wakati kukiwa na majibizano makali pia.

Kwenye matamshi yaliyotolewa kwa njia ya televisheni wakati wa mkutano wa kimataifa wa usalama kwenye chuo kikuu cha Reichman, waziri Gallant alionyesha picha za kile alitaja kuwa uwanja wa ndege uliojengwa na Iran kwa madhumuni ya kigaidi dhidi ya Israel. Ingawa hakutoa maelezo zaidi, picha hizo zilichukuliwa karibu na kijiji cha Lebanon cha Birket Jabbour na mji wa Jezzine, uliopo kilomita 20 kaskazini mwa mji wa mpakani wa Israel wa Metulla.

Kufikia sasa hakuna tamko lolote lililotolewa na Hezbollah wala Iran kufuatia madai hayo.

Forum

XS
SM
MD
LG