Wachambuzi wanasema hakuna uwezekano wa mabadiliko yoyote makubwa katika uhusiano wa mataifa ya Asia kusini mashariki na Beijing.
Hata hivyo, wasiwasi kuhusu usalama wa wafanyakazi na uchafuzi wa mazingira unaohusishwa na uwekezaji wa China, pamoja na madai ya Beijing, katika bahari ya South China, yatautia majaribuni uthabiti wa uhusiano huo.
Wakati rais Joko Widodo, alipokuwa madarakani, China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Indonesia, ikitumia rasilimali zake tajiri.
Jokowi, kama anavyoitwa mara nyingi, ameitaka China, kuwekeza zaidi Indonesia na amekuwa mshirika mkuu katika mpango wake wa miundombinu wa BRI.
Forum