Zoezi hilo linatarajiwa kuwa na ushindani wa wagombea watatu, Subianto kamanda wa zamani wa jeshi akielezewa kuwa ana nafasi kubwa ya kushinda.
Karibu wakazi milioni 205 wa Indonesia, theluthi moja wakiwa vijana wa chini ya umri wa miaka 30, wanatarajiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo wa rais na bunge, utakaofanyika Februari 14 mwaka ujao, kwenye taifa hilo la tatu kwa ukubwa ulimwenguni.
Maelfu ya watu wamejitokeza Jumatano kumshangilia Prabowo mwenye umri wa miaka 72, na Raka wakati walipokuwa wakiwasilisha nyaraka zao pamoja na manifesto kwa maafisa wa uchaguzi katika mji mkuu wa Jakarta.
Forum