Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 12:03

Wakenya waomboleza kifo cha George Saitoti


Wafanyakazi wa shirika la Msalaba Mwekendu Kenya wakifukua mabaki ya maiti za watu sita waliokufa katika milima ya Ngong, Nairobi, June 10, 2012.

Kenya yaomboleza vifo vya mawaziri wake

Kenya imetangaza siku tatu za maombolezibaada ya kifo cha waziri wa Usalama wa Ndani Profesa George Saitoti na naibu wake Joshua Orwa Ojodeh, kwenye ajli ya helikopta ya polisi kwenye msitu wa Ngong nje ya mji wa Nairobi.

Rais Mwai Kibaki alisema kifo cha Bwana Saitoti ni msiba mkubwa kwa taifa, na serikali imetangaza kuwa baraza la mawaziri litakutana Jumatatu, kujadili tukio hilo

Maafisa wa Kenya wanasema Profesa Saitoti ni miongoni mwa watu sita waliokufa baada ya helikopta ya polisi kuanguka mapema Jumapili karibu na mji mkuu wa Nairobi.

Maafisa wanasema naibu waziri wa Usalama wa Ndani Joshua Orwa ojodeh pia alifariki katika ajali hiyo ya helikopta iliyotokea katika milima ya Ngong. Marehemu George Saitoti ambaye alikuwa zamani makamu rais wa Kenya alikuwa ana mpango wa kuwania kiti cha

Pamoja na waziri Saitoti na naibu wake Ojodeh, marubani wao Nancy Gatuanja na Luke Oyugi walifariki dunia katika ajali hiyo. Pia walinzi wa mawaziri hao walipoteza maisha yao.

Mara tu baada ya ripoti za ajali hiyo kutokea, rais wa Kenya Mwai Kibaki alihutubia taifa kwa njia ya televisheni akieleza masikitiko yake makubwa na msiba uliokumba taifa lake kwa kupoteza maafisa wake.

Miongoni mwa maafisa wa ngazi ya juu waliofika kwenye mahala pa ajali hiyo ni Waziri Mkuu Raila Odinga na Makamu rais wa Kenya bwana Kalonzo Musyoka.

XS
SM
MD
LG