Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 04:56

Waziri wa Fedha wa Uingereza azindua Bajeti, mgomo wa wafanyakazi waendelea


Britain's Chancellor of the Exchequer Jeremy Hunt holds the budget box on Downing Street in London, March 15, 2023.
Britain's Chancellor of the Exchequer Jeremy Hunt holds the budget box on Downing Street in London, March 15, 2023.

Waziri wa Fedha wa Uingereza amewasilisha mpango wa bajeti yake siku ya Jumatano huku  wafanyakazi katika sekta mbalimbali wanaendelea na mgomo ili kufikisha ujumbe kuhusu dosari zilizokuwepo katika mishahara  na mfumuko wa bei.

Jeremy Hunt amejitayarisha kwenda mbele ya bunge na kutangaza vipi anakusudia kuboresha ukuaji wa uchumi nchini Uingereza.

Hunt amepuuza wito wa kupunguza kodi na tayari ametangaza dola 6.1 bilioni katika matumizi mapya ya ulinzi na ufadhili zaidi wa huduma ya watoto.

Serikali hiyo pia imekataa madai kutoka kwa wafanyakazi wa sekta ya umma kuongezwa mishahara kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha, akisema mishahara hiyo ya juu itapelekea kuongezeka zaidi kwa mfumuko wa bei.

Wafanyakazi wameshikilia madai yao, na siku ya Jumatano walimu, madereva wa treni, wafanyakazi wa serikali na madaktari vijana walikuwa wanagoma ili kutaka wasikilizwe kwa kile wanachosema ni nyongeza muhimu ya mishahara.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

XS
SM
MD
LG