Waziri wa fedha wa Scotland Kate Forbes amesema Jumatatu kwamba atawania kinyang’anyiro cha uongozi kuchukua nafasi ya Nicola Sturgeon kama kiongozi wa chama cha Scottish National Party (SNP) na Waziri Mkuu wa Scotland.
Forbes alichaguliwa na bunge la Scotland mwaka 2016 aliingia madarakani kama waziri wa fedha miaka minne baadae alikuwa mgombea wa tatu kutangaza nia yake ya kuwania nafasi ya uongozi katika SNP baada ya kujiuzulu ghafla kwa Sturgeon wiki iliyopita.
Kuondoka kwa Sturgeon kumeacha swali juu ya mapambano ya SNP ya uhuru wa Scotland wakati serikali ya Westminster inakwamisha juhudi zao za kuitisha kura ya pili baada ya kura ya maoni ya mwaka 2014 wakati Scottland ilipopiga kura asilimia 55 kwa 45 kuendelea kuwa sehemu ya Uingereza.
Facebook Forum