Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 06, 2025 Local time: 16:50

Waziri Mkuu wa zamani wa Tunisia amekamatwa na polisi nchini humo


Waziri Mkuu wa zamani wa Tunisia, Ali Larayedh
Waziri Mkuu wa zamani wa Tunisia, Ali Larayedh

Larayedh ambaye alihudumu kama Waziri Mkuu kutoka 2013 hadi 2014 alikamatwa kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya kuhusika katika kuondoka kwa maelfu ya vijana wa Tunisia kwenda kupigana na makundi ya kijihadi nje ya nchi

Polisi nchini Tunisia wamemkamata Waziri Mkuu wa zamani Ali Larayedh, chama chake cha Ennahdha chenye kufuata misingi ya kiislamu kimesema Jumanne, kikishutumu maafisa wa serikali kwa kujaribu kugeuza hali ya mambo kutokana na miito ya kumtaka Rais Kais Saied kujiuzulu.

Kukamatwa kwa kiongozi wa pili wa Ennahdha kunajiri siku chache baada ya karibu asilimia 90 ya wapiga kura kususia uchaguzi wa bunge jipya lisilo na nguvu lililoundwa na Saied kufuatia kuzuiwa kwake kuwa na mamlaka makubwa mwaka 2021.

Larayedh, ambaye alihudumu kama waziri mkuu kutoka 2013 hadi 2014, alikamatwa kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya kuhusika katika kuondoka kwa maelfu ya vijana wa Tunisia kupigana na makundi ya kijihadi nje ya nchi.

Takriban Wa-tunisia 6,000 walisafiri kwenda Libya, Iraq na Syria kwa kujitolea kama wapiganaji wa kigeni, idadi ambayo makundi kadhaa ya upinzani duniani yanasema yanaonyesha kupuuzwa kwa makusudi.

Uchunguzi huo ambao pia umemlenga kiongozi mkongwe wa chama cha Ennahdha Rached Ghannouchi, ulianzishwa baada ya rais huyo anayepinga vikali Uislamu kuifuta serikali na kulisimamisha bunge hapo Julai 2021.

Saied ametetea unyakuzi wake wa madaraka kuwa muhimu ili kumaliza mizozo ya mara kwa mara ya kisiasa iliyoambatana na kipindi cha mpito cha nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika kuelekea demokrasia kufuatia mapinduzi ya kwanza ya kiarabu ya mwaka 2011.

XS
SM
MD
LG