Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 20:04

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan afunguliwa rasmi mashtaka ya kutoa siri za serikali


Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan

Mahakama maalum ya Pakistan leo imemfungulia mashitaka Imran Khan waziri mkuu wa zamani aliyefungwa jela, pamoja na naibu wake kuhusiana na shutuma zenye utata za kuvujisha  siri za serikali.

Jopo la mahakama limesikiliza kesi hiyo kwa faragha ndani ya jela iliyoko karibu na mji mkuu wa Islamabad, kwa mujibu wa sheria ya kikoloni kuhusu siri za serikali. “Kikao cha leo kilikuwa cha kuwafungulia mashitaka, ndiyo maana wakasomewa mbele ya mahakama,” amesema mwongoza mashitaka maalum Shah Khawar, aliwaambia wanahabari nje ya jela ya Adiala.

Amesema kwamba mahakama imeanza rasmi kusikiliza kesi hiyo na kwamba mashahidi watakuwepo kwenye usikilizaji wa Ijumaa. Khan mwenye umri wa miaka 70 na mshtakiwa mwenza Shah Mahmood Qureshi ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Pakistan, wamekana mashitaka hayo, mawakili wao wamesema. Wameongeza kusema kwamba wameapa kupinga mashitaka hayo kwenye mahakama ya juu.

Forum

XS
SM
MD
LG