Maiga,mwenye umri wa miaka 68, alikamatwa mwezi Agosti kwa kushukiwa kuhusika katika ununuzi wa ndege ya rais wakati wa utawala wa rais wa zamani Ibrahim Boubacar Keita, aliyeondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi mwaka mmoja kabla.
Alishtakiwa kwa makosa kadhaa ya ufisadi na alikuwa akisubiri kesi. Wanasheria wake walisisitiza kuwa mteja wao hakuwa na hatia.
Mmoja wao aliambia Reuters kuwa alifariki katika kliniki katika mji mkuu Bamako siku ya Jumatatu asubuhi, ambapo alikuwa amelazwa hospitalini baada ya kupata msamaha wa kutoka jela tangu Desemba.
Familia yake na madaktari walikuwa wamejaribu bila mafanikio kwa Maiga kuruhusiwa kusafiri nje ya nchi kwa matibabu huku afya yake ikizorota katika gereza kuu la Bamako.