Muhyiddin alikamatwa kwenye makao makuu ya tume ya kupambana na ufisadi ya Malaysia, baada ya kujifikisha kwa mahojiano kuhusu kesi ya ufisadi inayoendelea dhidi yake.
Kupitia taarifa, tume hiyo imesema kwamba kiongozi huyo atafunguliwa mashtaka kadhaa Ijumaa, chini ya sheria za ufisadi kuhusiana na mradi wa Jana Wibawa unaohusishwa na mabilioni ya dola za kuwasaidia wakandarasi wa makabila ya Malay, pamoja na makundi mengine ya walio wachache, wakati wa janga la Covid-19. Waziri huyo zamani amekanusha madai hayo na badala yake kusema kwamba yana ushawishi wa kisiasa.