Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 01:46

Tunisia: Waziri mkuu kuteua watu wasio wanasiasa kuwa mawaziri


Waziri mkuu mteule wa Tunisia Hichem Mechichi,

Waziri mkuu mteule nchini Tunisia amesema kwamba ataunda baraza la mawaziri lenye watu ambao sio wanasiasa kufuatia mzozo usiomalizika kati ya vyama vya kisiasa kuhusu uundwaji wa serikali mpya.

Hatua ya Hicehm Mechichi, huenda ikamuweka katika hali ya mvutano na chama cha Ennahda chenye wabunge wengi na ambacho tayari kimesema kwamba kitapinga kabisa hatua yoyote ya kuteua serikalini watu ambao sio wanasiasa.

Hata hivyo pendekezo la kuunda serikali ya wataalam wasioegemea kundi lolote la kisiasa huenda likapata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa muungano wa wafanyakazi wenye nguvu sana nchini Tunisia -UGTT, Pamoja na vyama vingine vya kisiasa, vikiwemo Tahya Tounes na Dustoury el Hor.

Mechichi amesema kwamba lengo la serikali litakuwa kutatua hali ngumu ya maisha wanaopitia watu wa kawaida na kujenga uchumi ambao umeharibika.

Amekashifu wanasiasa kwa kuzozana wakati raia wa kawaida hata hawana maji safi ya kunywa.

Maandamano yametokea katikati mwa Tunisia mwaka huu kulalamikia ukosefu wa ajira na huduma mbovu serikalini hasa za afya, ukosefu wa maji na umeme.

-Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG