Waziri Mkuu wa Singapore Lee Hsien Loong ametangaza Jumapili atakabidhi madaraka kwa kizazi cha viongozi vijana kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025.
Lee mwenye miaka 71 alipanga kujiuzulu ifikapo mwaka 2022 kabla ya kutimiza miaka 70 ya kuzaliwa kwake, na kukabidhi madaraka kwa naibu wake, Lawrence Wong. Lakini hilo liliahirishwa huku Lee akisema kuwa alilazimika kuiongoza Singapore kupitia janga la virusi vya corona.
Katika hotuba yake kwa wanachama wa chama chake cha People's Action Party (PAP) leo Jumapili, Lee alisema Wong na timu yake “wameimarika ki-uongozi wakati wa janga hilo na “hakuna sababu ya kuchelewesha kipindi cha mpito cha kisiasa”. “Kwa hiyo, ninakusudia kumkabidhi DPM Lawrence kabla ya uchaguzi mkuu ujao”, Lee alisema.
“Baada ya hapo, nitakuwa kwenye nafasi mpya ya Waziri Mkuu. Nitakwenda popote anapofikiri ninaweza kuwa na manufaa. Nitafanya kila niwezalo kumsaidia yeye na timu yake kupambana na kushinda uchaguzi mkuu ujao”, alisema.
Forum