Ghasia zilizuka kwenye mji mkuu wa Port Moresby Jumatano jioni, baada ya kundi la wanajeshi, maafisa wa polisi pamoja na walinzi wa jela kuanzisha maandamano dhidi ya serikali. Baada ya saa kadhaa, maandamano hayo yalikuwa yameenea hadi kwenye mji wa Lae uliopo takriban kilomita 300 upande wa kaskazini.
Marape ameomba msamaha kwa taifa mapema leo akisema kwamba uvunjifu wa sheria hautovumiliwa. “Hii ni nchi yenu sawa na ilivyo yangu. Kuvunja sheria hakutaleta matokeo yoyote,” amesema Marape. Mkuu wa polisi David Manning amethibitisha kuwa takriban watu 15 wamekufa wakati wa maandamano hayo.
Hospitali kuu ya Port Morsby imetibu watu 25 kutokana na majeraha ya risasi, kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la habari la AFP, wakati watu wengine 6 wakiripotiwa kuwa na majeraha ya kuchomwa visu.
Forum