Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 23:19

Waziri mkuu wa Pakistan atakiwa kujiuzulu


Mpinzani mkuu wa kisiasa nchini Pakistan, Imran Khan, amemtaka Waziri Mkuu wa nchi hyo Nawaz Sharif kujiuzulu.

Shauri hilo limetolewa baada ya nyaraka zilizotolewa kwa siri na kituo cha sheria cha Panama kufichua kwamba watoto wake mwenyewe wanamiliki kampuni kadhaa katika nchi ya nje.

Ufichuaji huo umezua mjadala mkubwa nchini Pakistan katika duru za kisiasa na vyombo vya habari ukimkosoa waziri mkuu Sharif kwa kudaiwa kuficha mali za familia yake kwa siri.

Waziri mkuu huyo amepinga madai yoyote ya uwajibikaji wake ama wa watoto wake wa kiume usio sahihi.

Wiki iliyopita alitangaza kuanzishwa kwa tume ya sheria itakayoongozwa na jaji mstaafu kuchunguza kashfa hiyo.

Lakini mpinzani wake mkuu Imran Khan, katika hotuba kupitia televishani amepinga kuundwa tume hiyo akisema ni jaribio la kuficha ulaji rushwa umaofanywa na familia ya Sharif.

XS
SM
MD
LG