Viongozi kadhaa wa dunia walitoa heshima zao kwa ubora wa uongozi wake na kuwa mwanasiasa asiyependa mchezo. Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese alitweet: "Jacinda Arden, ambaye aliionyesha dunia jinsi ya kuongoza kwa akili na nguvu.”
Jacinda Arden, ambaye huruma yake katika kukabiliana na tukio la ufyatuaji risasi lililoua watu wengi na majibu yake kwa janga la virusi vya corona yalipelekea kuwa kiongozi wa kimataifa, lakini alikabiliwa na ukosoaji mwingi nyumbani, alisema Alhamisi kuwa anaondoka madarakani.
Tangazo lake limekuja kama mshtuko kote katika taifa hilo lenye watu milioni tano.
Akijizuia kulia, Arden aliwaambia wana habari huko Napier kwamba Februari 7 itakuwa ni siku yake ya mwisho kama waziri mkuu.
Jacinda Arden, Waziri Mkuu wa New Zealand aneleza: “Ninaingia mwaka wa sita madarakani, na kila wakati katika miaka hiyo, nimejitolea kabisa. Naamini kwamba kuiongoza nchi ni fursa kubwa sana kwa mtu yeyote ambaye amewahi kuifanya, lakini pia ina changamoto nyingi. Huwezi na si rahisi kuwa utaweza labda liwe tanki limejaa, na una ziada ya kukabiliana na changamoto ambazo hazikutarajiwa.
Majira ya joto mwaka huu, nilikuwa na matumaini ya kujitayarisha kwa raundi nyingine, lakini awamu nyingine kwasababu ndiyo ilikuwa inatakiwa iwe hivyo mwaka huu. Sijaweza kufanya hivyo. Kwa hiyo hivi leo, natangaza kwamba sitawania kuchaguliwa tena na awamu yangu kama waziri mkuu itamalizika rasmi Februari 7. Miaka hii mitano na nusu imekuwa ni yenye shughuli nyingi katika maisha yangu, lakini pia ilikuwa na changamoto zake.”
Adern amekuwa ni kivutio kwa wanawake kote duniani baada ya kushinda nafasi hiyo ya juu mwaka 2017 akiwa na umri mdogo wa miaka 37.
Mwaka uliofuata, alikuwa ni kiongozi wa pili tu duniani kujifungua akiwa madarakani.
Mwaka 2019, Arden alikabiliwa na moja ya siku zenye giza nene katika historia ya New Zealand wakati mzungu mwenye msimamo wa kibaguzi alipovamia misikiti miwili huko Christchurch nakuwaua watu 51.
Alipongezwa sana kwa jinsi alivyowakumbatia manusura na jamii ya Waislamu New Zealand baada ya tukio hilo.
Christopher Luxon, Kiongozi wa Upinzani, New Zealand anaeleza: “Ningependa kukiri na kumshukuru waziri mkuu kwa huduma zake kwa nchi yetu. Sitaki kusema kwamba najivuna kwa kuchukua kazi nzito na kwa hakika amejitahidi kwa kadri ya uwezo wake.
Nadhani ninapoangazia hilo, naweza kusema jinsi alivyoiongoza New Zealand kupitia mashambulizi ya kigaidi ya Christchurch kwa njia ambayo tulihisi ni kujivunia kwa majibu kutoka kwa nchi na kutoka kwake kama kiongozi wetu, na kwa njia ambayo siku zote amekuwa balozi mzuri katika ulimwengu ni mambo ambayo kwa kweli yatakuwa ni urithi wake muhimu, na namuombea mema yeye na familia yake kwa siku za usoni.”
Ingawaje kumekuwepo na baadhi ya maoni kutoka kwenye duru za kisiasa ambazo zinasema kuhusu Adern anajiuzulu kabla ya uchaguzi ujao, wakati ambapo aliwahi kusema kuwa anapanga kuwania tena.
Waziri wa Fedha wa Australia Jim Chalmers ambaye chama chake cha Labor kina uhusiano na chama tawala cha New Zealand amemuelezea Arden kama mtu mkarimu.
Jim Chalmers, Waziri wa Fedha wa Australia anaeleza: “Jacinda Arden ambaye anaongoza na kutawala kwa njia yake mwenyewe na hivi sasa anaondoka kwa misingi yake. Urafiki wake kwa hakika ni mpana na wa kina kuliko mtu yeyote, lakini Jacinda Arden, ni waziri mkuu wa kipekee.
Tunazunguma kuhusu chanzo cha nguvu nyumbani New Zealand na chanzo cha msukumo mkubwa kote duniani. Jacinda Ardern ni zaidi ya rafiki kwa Australia, ni kama dada. Baadhi yetu tuna bahati kubwa ya kukutana naye na kufanya kazi na mawaziri wake, lakini ilikuwa huna haja ya kumfahamu binafsi kujihisi unamjua Jacidan Adern.
Adern alisema hana mipango yoyote hivi sasa baada ya kuondoka madarakani, mbali na kukaa na familia yake na mtoto wake wa kike Neve, na mchumba wake Clarke Gayford, baada ya mlipuko wa virusi vya corona kuvuruga mipango yake ya mapema ya harusi.
Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.