Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe, atakuwa kiongozi wa kwanza duniani kukutana na rais mteule wa Marekani, Donald Trump.
Wawili hao wamepanga kufanya mazungumzo Alhamisi, mjini New York, lakini haija-fahamika muda na mahala watakapo kutana.
Abe alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa kwanza kumpigia simu Trump, kumpongeza baada ya kushinda uchaguzi wa rais wa wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa afisa wa juu wa serekali ya Japan, Abe alimwambia Trump, kwamba ushirikiano madhubuti wa Marekani na Japan ni muhimu katika kuhakikisha amani katika ukanda wa Asia-Pacific.
Trump alishutumu vikali kuhusu Japan na mataifa ya Asia, akitaka kuwajibika zaidi katika kufadhili ulinzi wa eneo la Asia-Pacific, ikijumuisha gharama za kuhudumia kambi za kijeshi za Marekani zilizopo Japan.