Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:10

Netanyahu akanusha madai ya kutaka kuuliwa


Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamini Netanyahu, na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamini Netanyahu, na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamini Netanyahu, leo amekanusha ripoti kwamba maisha yake yalikuwa hatarini wakati wa ziara yake nchini Kenya wiki hii.

Kulingana na shirika la habari la 'Associated Press', Netanyahu amewaambia waandishi wa habari mjini Addis Ababa, Ethiopia, kwamba hakujua lolote kuhusu jaribio la kumuua na kwamba alisikia madai hayo kwa mara ya kwanza alipoulizwa swali hilo na mwandishi wa habari mjini Addis Ababa.

Waziri Mkuu wa Israel hupewa ulinzi mkali akiwa nje na ndani ya nchi yake, hususan kwa sababu ya vitisho vingi dhidi ya Israeli ulimwenguni kote. Aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Yitzak Rabin, aliuawa na mwanamgambo wa kiyahudi mjini Tel Aviv mwaka 1995.

Ziara hiyo ya Netanyahu ya mataifa manne katika bara la Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ni ya kwanza kwa karibu miongo mitatu kufanywa na Waziri Mkuu wa Israel aliye mamlakani.

XS
SM
MD
LG