Waziri Mkuu wa Iraq amefanya mazungumzo na Rais wa Syria Bashar al-Assad mjini Damascus wakati wa ziara yake ya kwanza ya aina yake katika taifa hilo lililokumbwa na vita tangu kuanza kwa vita vya miaka 12.
Iraq na Syria zimekuwa na uhusiano wa karibu kwa miaka kadhaa hata baada ya nchi nyingi za Kiarabu kuwaondoa mabalozi wao mjini Damascus, na uanachama wa Syria kusimamishwa katika jumuiya ya mataifa ya kiarabu yenye nchi wanachama 22 kutokana na ukandamizaji wake dhidi ya waandamanaji mwaka 2011.
Assad alimpokea Mohammed Shia al-Sudani, ambaye alikuwa akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu, katika makazi ya rais mjini Damascus. Walijadili uhusiano wa pamoja na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili jirani, miongoni mwa masuala mengine, kulingana na ofisi ya rais wa Syria.
Ofisi ya Al-Sudani imesema katika taarifa yake kwamba mazungumzo yalihusu njia za kupanua ushirikiano katika nyanja za biashara, uchumi, usafirishaji, utalii, namna ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, na ushirikiano wa kupambana na ugaidi.
Forum