Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Agosti 26, 2026 Local time: 02:13

Waziri Mkuu wa Canada awataka raia wa nchi yake walioko Lebanon wajiandikishe kusafirishwa nyumbani

Waziri Mkuu wa Kanada Justin Trudeau akizungumza na waandishi wa habari kabla ya Kipindi cha Maswali katika ukumbi wa House of Commons bungeni  huko Ottawa.
Waziri Mkuu wa Kanada Justin Trudeau akizungumza na waandishi wa habari kabla ya Kipindi cha Maswali katika ukumbi wa House of Commons bungeni huko Ottawa.

Canada ina raia  6,000 waliojiandikisha kuondoka nchini humo na maafisa wanajaribu kufikia wengine 2,500 mwishoni mwa juma,

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau aliwataka raia wa nchi yake ambao bado wako Lebanon Jumamosi wajiandikishe kusafirishwa kwa ndege maalum ambazo tayari zimesaidia zaidi ya raia 1,000 kuondoka, huku hali ya usalama ikizidi kudorora.

Canada ina raia 6,000 waliojiandikisha kuondoka nchini humo na maafisa wanajaribu kufikia wengine 2,500 mwishoni mwa juma, afisa katika ofisi ya Trudeau alisema akiongeza kuwa safari zaidi za ndege zilikuwa zikiongezwa kwa siku ya Jumatatu na Jumanne.

"Bado tuna nafasi kwenye ndege zilizoandaliwa na Canada. Tunawahimiza Wa Canada wote kuchukua nafasi kwenye ndege hizi na kuondoka Lebanon wakati bado wanaweza kufanya hivyo” Trudeau alisema katika mkutano wake na viongozi kutoka nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa nchini kwake.

This item is part of

Forum

XS
SM
MD
LG