Majukwaa mbadala ni kama vile Telegram na TikTok, lakini bado hakujakuwa na mabadiliko makubwa. Hun Sen alifuta ukurasa wake Juni 29 baada ya bodi inayosimamia Facebook na Instagram kutangaza kwamba alichochea ghasia na k hivyo kumfungia ukurasa huo kwa muda wa miezi 6.
Tangu wakati huo, Sen amekuwa akituma ujumbe wake kupitia Telegram ambako ana wafuasi 975,000 ikilinganishwa na 850,000 aliokuwa nao mwishoni mwa Juni. Akaunti yake mpya ya TikTok imejikuta ikiwa na takriban wafuasi 244,000, wakati pia akianza tena kutumia Twitter kwa mara ya kwanza baada ya mwaka mmoja.
Forum