Sasa Truss anakabiliwa na uasi ndani ya Chama tawala cha Conservative ambao unaacha uongozi wake ukining'inia kwenye kamba. Mbunge wa kihafidhina Robert Halfon aliishutumu serikali hiyo Jumapili kwa kuichukulia nchi hiyo kama “panya wa maabara ambao wanaweza kufanyiwa majaribio ya juu ya soko huria."
Wahafidhina wanatafakari iwapo wajaribu kumfukuza kiongozi wao. Truss, wakati huo huo, amemteua waziri mpya wa Fedha , Jeremy Hunt, ambaye anapanga kubadili kwa kiasi kikubwa mpango wake wa kiuchumi atakapotoa taarifa ya bajeti Oktoba 31.