Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:49

Waziri mkuu Abbiy asema ataongoza wanajeshi wake katika uwanja wa vita


Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akizungumza katika kikao nchini Ethiopia.
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akizungumza katika kikao nchini Ethiopia.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anasema sasa atawaongoza wanajeshi wake katika uwanja wa vita  huku mzozo wa mwaka mzima ukikaribia mji mkuu, Addis Ababa.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anasema sasa atawaongoza wanajeshi wake katika uwanja wa vita huku mzozo wa mwaka mzima ukikaribia mji mkuu, Addis Ababa.

Kuanzia kesho, nitakuwa mbele ili kuongoza vikosi vya ulinzi, Bw Abiy, alisema katika taarifa iliyochapishwa kwenye Twitter Jumatatu jioni.Wale wanaotaka kuwa miongoni mwa watoto wa Ethiopia, watakaosifiwa na historia, inukeni kwa ajili ya nchi yenu leo. Tukutane mbele, aliongeza.

Ilikuja baada ya kamati kuu ya chama tawala cha Prosperity Party kukutana siku ya Jumatatu kujadili vita hivyo. Waziri wa ulinzi aliviambia vyombo vya habari vya ndani baada ya mkutano huo kwamba vikosi vya usalama vitaanza hatua tofauti kuhusu mzozo huo.

Chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF) kimepuuza kauli ya Bw Abiy. Msemaji wake, Getachew Reda, alisema kwamba vikosi vyetu havitalegea katika harakati zao zisizoweza kuepukika kuelekea kukomesha tabia ya ukabaji ya Abiy kwa watu wetu.

Tangu Novemba mwaka jana, serikali na vikosi vya Tigray vimeshiriki katika vita vilivyoanza huko Tigray na kuenea katika mikoa jirani ya Amhara na Afar. TPLF imeunda muungano na vikundi vingine vya waasi likiwemo Jeshi la Ukombozi la Oromo (OLA) huku mzozo huo ukikaribia mji mkuu.

XS
SM
MD
LG