Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 28, 2023 Local time: 09:48

Waziri Gabon ajiuzulu


Waziri wa sheria wa Gabon, Seraphin Moundounga amejiuzulu kufuatia mgogoro baada ya rais wa nchi hiyo Ali Bongo, kuchaguliwa tena.

Waziri huyo anakuwa afisa wa kwanza wa ngazi ya juu kujiuzulu toka kumalizika kwa uchaguzi.

Tume ya uchaguzi ya Gabon ilimtangaza Bongo mshindi dhidi ya kiongozi wa upinzani Jean Ping kwa takriban kura 5,000.

Ushindi wa Bongo umezua maandamano na ghasia mitaani ambazo zimesababisha vifo vya watu sita.

Moundounga ameiambia Radio France International, Jumatatu kwamba serekali haishughulikii wasiwasi kuhusu haja ya kuwepo kwa amani na hivyo ameamua kujiuzulu.

Pia hapo jana kiongozi wa upinzani Ping, ambaye amejitangaza kuwa ni kiongozi wa Gabon, ametoa mwito wa mgomo wa wote akisema vizuizi vya kiuchumi vitatoa shinikizo kwa serikali.

Hata hivyo watu wachache walionekana kukaa majumbani huku maduka mengi na benki katika mji mkuu Libreville zikifunguliwa tena baada ya ghasia.

Baadhi ya wakazi wa mji wamesema hawakusikia mwito wa mgomo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG