Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 21:14

Waziri Blinken wa Marekani amehitimisha ziara yake Mashariki ya Kati


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken

Na muda ni kiini kikuu kwa sababu kila siku inayopita kuna hatari ya kuongezeka mapigano katika eneo la Gaza.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amehitimisha ziara yake ya tisa Mashariki ya Kati Jumanne jioni, akisema Israel na Hamas zinahitaji kufikia haraka makubaliano ya kusitisha mapigano.

“Wakati unakwisha kwa sababu kila siku inayopita ustawi na maisha ya mateka yako hatarini,” alisema kabla ya kuondoka Doha, Qatar. “Muda ni jambo la msingi kwa sababu kila siku wanawake, watoto, wanaume huko Gaza wanateseka bila kupata chakula cha kutosha, dawa, na wapo katika hatari ya kujeruhiwa au kufa katika mapigano ambayo hawakuya-anzisha na hawawezi kuyasitisha.

Na muda ni kiini kikuu kwa sababu kila siku inayopita kuna hatari ya kuongezeka mapigano kwa eneo hilo.” Baada ya kusafiri kwenda Israel mapema wiki hii, ambapo alisema Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alikubali pendekezo lililowasilishwa na wajumbe kutoka Marekani, Qatar na Misri, Blinken alikutana na maafisa mjini Cairo na Doha.

Forum

XS
SM
MD
LG