Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:13

Wazambia kupata Rais mpya


Wananchi wa Zambia wakipanga mstari katika uchaguzi wa Januari, 20, 2015.
Wananchi wa Zambia wakipanga mstari katika uchaguzi wa Januari, 20, 2015.

Wananchi wa Zambia wamepiga kura leo ili kuziba nafasi ya urais iliyoachwa wazi na marehemu Rais Michael Sata, aliyefariki dunia mwezi Oktoba mwaka jana.

Kuna wagombea kumi na moja wa nafasi hiyo, lakini wapinzani wakubwa ni Waziri wa ulinzi Edgar Lungu, wa chama cha marehemu Rais Sata Patriotic Front, na Hakainde Hichilewa anayeongoza chama cha upinzani cha United Party for National Development (UPND).

Mshindi katika uchaguzi ataongoza kwa mwaka mmoja na nusu kukamilisha muhula wa miaka mitano ya Bwana Sata, baada ya kufanikiwa kushinda katika uchaguzi wa mwaka 2011.

Uchaguzi wa muhula mpya wa Urais umepangwa kufanyika mwakani ili kumpata kiongozi wa Zambia katika kipindi cha miaka mitano.

Bwana Isaac Mwanza, mshauri wa maswala ya kidemokrasia na utawala katika mradi wa Rais Obama wa viongozi vijana wa Afrika (YALI) kwa upande wa Zambia, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba kampeni za bwana Lungu zinaendeleza mipango ya marehemu rais Sata.

XS
SM
MD
LG